Wadephul: Urusi inahatarisha amani na uhuru wa Ujerumani
29 Juni 2025Matangazo
Wadephul amesema Urusi inatishia moja kwa moja mfumo wa maisha yenye amani na uhuru yaliyopo Ujerumani.
Wadephul ameyasema hayo kupitia shirika la habari la Funke katika maoni yake yaliyochapishwa Jumapili, akivitaja vita vya Urusi dhidi ya Ukraine kuwa tishio kubwa zaidi la usalama barani Ulaya na suala muhimu zaidi katika sera ya kigeni ya Ujerumani.
Aidha waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani amepongeza maamuzi ya hivi karibuni ya Jumuiya ya kujihami ya NATO iliyochukuliwa katika mkutano wa kilele mjini The Hague-Uholanzi, ambapo nchi wanachama zilikubali kuongeza matumizi yao ya ulinzi hadi asilimia 5 ya Pato la Ndani la Taifa, akiitaja hatua hiyo kuwa "sahihi na muhimu."