MigogoroUlaya
Ujerumani na Ukraine kuimarisha ushirikiano wa ulinzi
30 Juni 2025Matangazo
Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul baada ya kukutana na mwenzake wa Ukraine Andrii Sybiha mjini Kiev, na baadaye akitarajiwa kukutana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Wadephul ambaye aliambatana na wawakilishi wa ngazi za juu wa makampuni ya ulinzi ya Ujerumani ameongeza kuwa wataendelea kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake na Urusi na kwamba ushirikiano kati ya Ujerumani na Ukraine ni kwa maslahi ya pande zote mbili.
Hayo yanajiri wakati Urusi ikizidisha mashambulizi yake, huku ikionekana pia kupata mafanikio kadhaa katika mstari wa mbele wa vita kwa kuyatwaa maeneo zaidi ya Ukraine.