Wadephul: Kitisho cha Urusi kwa Ujerumani kisipuuzwe
1 Julai 2025Wadephul ameyasema hayo kupitia shirika la habari la Funkekatika maoni yake yaliyochapishwa leo Jumapili, akivitaja vita vya Urusi dhidi ya Ukraine kuwa tishio kubwa zaidi la usalama barani Ulaya na suala muhimu zaidi katika sera ya kigeni ya Ujerumani.
Aidha waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani amepongeza maamuzi ya hivi karibuni ya Jumuiya ya kujihami ya NATO iliyochukuliwa katika mkutano wa kilele mjini The Hague-Uholanzi, ambapo nchi wanachama zilikubali kuongeza matumizi yao ya ulinzi hadi asilimia 5 ya Pato la Ndani la Taifa, akiitaja hatua hiyo kuwa "sahihi na muhimu."
Kukosolewa kwa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine
Mwanachama mwandamizi wa chama cha Kansela Friedrich Merz cha CDU, amemkosoa Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kufanya mashambulizi ya kiholela dhidi ya Ukraine, akiongeza kuwa uhuru wa taifa hilo ni jaribio muhumu katika kutatua matatizo yao wenyewe barani Ulaya.
Soma zaidi:Scholz aonya kuhusu mustakabali wa Ulaya
Wakati huo huo, mjadala unaendelea ndani ya chama cha mrengo wa kushoto Democratic Party (SPD), mshirika mdogo katika muungano huo serikali, kuhusu jinsi ya kushughulika na Urusi. Hata hivyo, katika mkutano wa mwishoni mwa juma wa chama hicho kiongozi wa chama Lars Klingbeil aliikataa mabadiliko yoyote katika sera kuelekea Moscow.