Wadephul ataka ushirikiano na Marekani dhidi ya Urusi
28 Mei 2025Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kupanda ndege mjini Berlin kuelekea Washington, Wadephul amesema ili kumfanya Rais Putin wa Urusi kuja kwenye meza ya mazungumzo, lazima Marekani na Ulaya ziongeze mbinyo wao kwa Kremlin.
Wadephul anatazamiwa kukutana hivi leo na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Marco Rubio, kujadiliana mtazamo wa pamoja kuelekea mizozo ya sasa ya kimataifa.
Soma zaidi: Ujerumani yatafuta kuungwa mkono Ulaya bajeti ongezeko la ya ulinzi
Mbali ya suala la vita vya Urusi na Ukraine, mawaziri hao wawili wanatarajiwa kujadili hali ya mambo katika Ukanda wa Gaza, ambako janga la kibinaadamu lililosababishwa na mashambulizi ya Israel limezuwa ukosoaji mkubwa kutoka Berlin dhidi ya Tel Aviv.
Ujerumani na Marekani ni waungaji mkono wakubwa kijeshi, kifedha na kisiasa wa Israel.