Wademocrat wampinga Trump kuiuzia silaha UAE
16 Mei 2025Matangazo
Hatua hii ya maseneta wa chama cha Democratic inakuja muda mchache baada ya Rais Donald Trump kutangaza makubaliano mapya ya kibiashara ya dola bilioni 200 na taifa hilo la Ghuba.
Wanasiasa hao akiwemo Seneta Chris Murphy na Bernie Sanders ambaye si mwanachama wa Democratic ila anashirikiana nao, wamewasilisha maazimio ya kupinga taifa hilo la Ghuba kuuziwa silaha na Marekani kwa awamu tatu.
Maseneta hao wanasema kwamba kumekuwa na madai ya Abu Dhabi kuwahami wanamgambo wa RSF na silaha, madai ambayo taifa hilo limeyakanusha mara kadhaa.
Kwa upande Rais Donald Trump ametangaza mikataba hiyo ya kibiashara na Falme za Kiarabu huku akiahidi kuzidi kuimarisha mahusiano ya mataifa hayo mawili.