SiasaMali
Wadau wa siasa Mali wapendekeza Assimi Goita kuwa rais
30 Aprili 2025Matangazo
Mazungumzo hayo yalifanyika katika mji mkuu Bamako jana Jumanne, huku wajumbe wakipendekeza pia kufutwa kwa vyama vyote vya siasa pamoja na kuweka masharti magumu zaidi ya kuundwa kwa vyama vipya. Mapendekezo hayo yanatarajiwa kuanza kufanya kazi rasmi katika siku zijazo.
Kiongozi huyo aliyechukua mamlaka kufuatia mapinduzi ya mwaka 2021 katika nchi hiyo ya Sahel aliahidi kuandaa uchaguzi mwezi Februari mwaka 2022, lakini zoezi hilo liliahirishwa mara kadhaa. Mali imekuwa ikikabiliwa na changamoto za kiusalama kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ya makundi ya itikadi kali.