Wadau wa sekta ya habari Tanzania watoa wito wa usalama
29 Aprili 2025Maadhimisho hayo ya 33 tangu kuanzishwa kwake, yamewakusanya wadau muhimu wa habari na vyombo vya habari na kujadili mafanikio na changamoto mbali mbali ya sekta hiyo muhimu duniani.
Changamoto zinazowakabili wanahabari
Wadau wa habari pamoja na wanahabari wameainisha baadhi ya changamoto ambazo zinatakiwa kushughulikiwa na mamlaka kuwa ni pamoja na ulinzi wa wanahabari, elimu kwa wananchi kuhusu majukwaa ya kidijitali yatakayowawezesha kutambua vyanzo sahihi vya habari, pamoja na kupitiwa kwa sera ya utangazaji ya Tanzania ya mwaka 2003 kwa sababu haiendani na mazingira ya sasa ya kidijitali.
Serikali ya Tanzania imebainisha kwamba ipo tayari kushughulikia changamoto za wanahabari zitakazowasilishwa baada ya maadhimisho hayo, lakini ni jukumu la vyombo vya habari na wanahabarikuhakikisha vinaboresha taaluma hiyo ili kuendana na mabadiliko ya kidijitali yanayokua kwa kasi.
Kauli mbiu ya mwaka huu
Maadhimisho ya mwaka huu, yamebebwa na kauli mbiu inayosema ''Uhabarishaji kwenye dunia mpya, mchango wa akili bandia kwenye uhuru wa vyombo vya habari,'' kauli mbiu hii ikilenga fursa na changamoto za uhuru wa habarikatika enzi ya teknolojia ya akili mnemba, AI.