SiasaAfrika Kusini
Wachimba migodi haramu 1000 wakamatwa nchini Afrika Kusini
2 Agosti 2025Matangazo
Msemaji wa polisi wa jimbo la Mpumalanga, Donald Mdhluli, ameliambia shirika la Habari la AFP kwamba operesheni hiyo ya polisi, iliyoanza siku ya Jumatatu, ililenga uchimbaji madini wa siri pembezoni mwa kijiji cha Barberton kilicho karibu na mipaka ya Eswatini na Msumbiji.
Kukamatwa kwa watu hao kumefanyika chini ya mwaka mmoja baada ya operesheni kama hiyo iliyofanywa karibu na mji wa Stilfontein, magharibi mwa Johannesburg, ambako wachimba migodi 90 walipoteza maisha. Migodi ya eneo hilo ilifungwa mnamo mwezi Januari.
Kama katika operesheni ya Stilfontein, polisi karibu eneo la Barberton waliuzunguka mgodi huo haramu na kuzuia vifaa na mahitaji kuingizwa, na kisha kuwalazimisha waliokuwa ndani watoke nje.