Wabunge wa Ujerumani kupigia kura muswada tata wa uhamiaji
31 Januari 2025Matangazo
Muswada huo uliwasilishwa na muungano wa kihafidhina wa CDU/CSU.
Chama cha AfD kimeashiria kuupigia kura muswada huo ambao pia unaonekana kuungwa mkono na chama cha Free Democrats kinachopendelea wafanyabiashara pamoja na muungano mpya wa mrengo mkali wa kushoto wa Sahra Wagenknecht, BSW.
Soma pia: Mamia waaandamana Berlin dhidi ya CDU kuhusu kura ya uhamiaji
Ikiwa utapita, muswaada huo utaanzisha kile kitakachoitwa Sheria ya Vikwazo vya Uhamiaji.
Sheria hiyo itajumuisha kuondoa mchakato wa familia za wakimbizi kuungana nchini Ujerumani, na kutoa mamlaka zaidi kwa polisi wa mipakani kuwarejesha wahamiaji.