Wabunge wa Ujerumani wanatazamiwa kujadili hatua ya Kansela mtarajiwa Friedrich Merz kufanyia mageuzi makubwa sheria zinazozuia ukopaji - hatua muhimu inayofuata kwa wahafidhina wake kuweza kuunda serikali mpya ya mseto ya Ujerumani. Mshirika wao anayetarajiwa, SPD, kinaunga mkono mapendekezo hayo, lakini vyama hivyo viwili vinakosa theluthi mbili ya wingi wa kura zinazohitajika.