Wabunge Uingereza wakubali Palestine Action kuitwa magaidi
3 Julai 2025Matangazo
Hapo jana, wajumbe 359 wa Baraza la Chini la Bunge walipiga kura ya kuunga mkono pendekezo la kuliweka kundi hilo chini ya Sheria ya Ugaidi ya Mwaka 2000 dhidi ya 26 waliopinga.
Sasa hoja hiyo inatazamiwa kujadiliwa kwenye Baraza la Juu la Bunge hivi leo kabla ya kuwa sheria rasmi.
Endapo sheria hiyo itapitishwa, litakuwa kosa la jinai lenye adhabu ya kifungo cha hadi miaka 14 jela kwa mtu kuwa mwanachama wa kundi hilo au hata kuliunga mkono.
Hata hivyo, kundi hilo limefunguwa kesi mahakamani kupinga hatua ya serikali kulitangaza kuwa la kigaidi na kesi hiyo inatazamiwa kusikilizwa kesho Ijumaa.