Jamii ya Baganda sio tu inawapa nafasi kubwa watoto mapacha lakini hata wazazi waliobahatika kupata mapacha huwekwa katika tabaka la juu ndani ya jamii. Wahafidhina wa mila za Baganda wanahisi ni baraka kupata mapacha na hivyo mama wa Kibaganda anapojifungua mapacha la kwanza kabisa ni kutoa habari kijijini juu ya ujio huo wa mapacha. Fahamu zaidi katika Utamaduni na Sanaa na Saumu Mwasimba.