Waasi wa M23 waendeleza mashambulizi mashariki ya Kongo
6 Februari 2025Maafisa wa mashirika ya kijamii na wakaazi wamesema waasi hao wa M23 wamekamata mji wa madini wa Nyabibwe, kilomita 100 kutoka mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini wa Bukavu. Mji wa Nyabibwe upo katikati ya Bukavu na Goma, mji ambao waasi hao waliukamata wiki iliyopita.
Naibu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo Vivian van de Perre amesema mji wa Goma bado umekaliwa na waasi wa M23 na mapigano makali yanaendelea kwenye barabara kuu ya kuelekea Bukavu.
Kongo yasema tangazo la M23 la usitishaji mapigano ni "mawasiliano ya uongo"
Wakati huo huo, maafisa wa serikali ya Kongo wametoa hati ya kimataifa ya kukamatwa Corneille Nangaa, mmoja wa viongozi wa kisiasa wa M23.
Nao waendesha mashitaka wa mahakama ya kimatiafa ya uhalifu wa kivita ICC mjini The Hague wamesema wanafuatulia kwa karibu hali katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakitambua vyanzo vya kuaminika vimesema mamia ya watu wameuliwa katika machafuko ya hivi karibuni.