MigogoroYemen
Wahouthi wawaachilia huru wafungwa wa kivita wapatao 153
25 Januari 2025Matangazo
Hii ni sehemu ya juhudi zao za kupunguza mvutano baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza. Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu ICRC imepongeza uamuzi wa kuachiliwa kwa watu hao na kusema ni hatua chanya kuelekea kufufua mchakato wa mazungumzo ya amani ili kumaliza vita vya muda mrefu nchini humo.
Hata hivyo, waasi hao wa Kihouthi wanaendelea kuwazuia wafanyakazi saba wa Umoja wa Mataifa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ametoa wito wa kuachiliwa huru mara moja na bila masharti, akisema kuendelea kuzuiliwa kwao kinyume na sheria hakukubaliki na kunaathiri vibaya uwezo wao wa kuwasaidia mamilioni ya watu wanaohitaji msaada nchini Yemen.