Waasi wa ADF wauwa zaidi ya watu 40 DR Kongo
28 Julai 2025Matangazo
Waasi wa ADF walilivamia Kanisa moja wa Kikatoliki kwenye mji wa Komanda, ambako waumini walikuwa wamekusanyika kwa ibada. Uvamizi huo ulipelekea mauaji ya watu 43, wakiwemo watoto tisa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Naibu mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo, Vivian van de Perre, amelaani mashambulizi hayo akiyaita uvunjaji wa haki za kibinaadamu na sheria za kiutu za kimataifa.
Mara ya mwisho kwaADF kufanya mashambulizi makubwa kama haya ilikuwa mwezi Februari, ambapo iliuawa watu 23 kwenye jimbo la Mambasa.
Licha ya operesheni ya pamoja ya kijeshi kati ya Kongo na Uganda, kundi hilo la waasi limeendelea kufanya mashambulizi makubwa kwenye majimbo ya mashariki mwa Kongo.