MigogoroAfrika
Mashambulizi ya ADF yawaua raia 66 Kongo
13 Julai 2025Matangazo
Kulingana na taarifa iliyotolewa Jumamosi na msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Ituri Jean Tobie Okala, takriban raia 30 waliuawa kati ya Alhamisi na Ijumaa wiki hii na idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia watu 66.
Mwenyekiti wa asasi moja ya kiraia, Marcel Paluku amebainisha kuwa watu hao waliuawa kwa mapanga huku wengine ambao idadi yao haijulikani wametekwa nyara. Shambulio hilo linashukiwa kuwa ni la kulipa kisasi dhidi ya mashambulizi yanayoongezeka dhidi ya waasi hao yanayofanywa kwa ushirikiano wa majeshi ya Kongo na Uganda.