MigogoroColombia
Waasi ELN waonya juu ya kuvurugika kwa mpango wa amani
10 Machi 2025Matangazo
Makamanda wawili wa kundi la waasi la Jeshi la Ukombozi wa Kitaifa la Colombia, ELN wamesema kwenye mahojiano ya nadra na AFP yaliyofanyika kwenye eneo ambalo halikuwekwa wazi kwamba hawatasita kupigana na wanajeshi 10,000 wa serikali waliokusanyika karibu na eneo walilopo.
Kundi hilo, al maarufu ELN, limeendesha uasi wa mrengo wa kushoto kwa miaka 60 dhidi ya serikali ya Colombia, na kunyakua maeneo mengi .
Tangu Januari, mapigano kati ya ya ELN na kundi pinzani la waasi katika eneo la mpaka la Catatumbo yamesababisha karibu watu 56,000 kuyahama makazi yao na karibu watu 76 kuuawa.
Yalikuwa ni machafuko makubwa zaidi kutokea nchini Colombia tangu makubaliano ya amani yalipofikiwa mwaka 2016.