Waandishi kadhaa wakamatwa Uturuki
25 Machi 2025Mamlaka ya Uturuki zimewakamata waandishi kadhaa wa habari siku ya Jumatatu kama sehemu ya shinikizo dhidi ya maandamano yaliyoibuka baada ya kumshikilia Meya wa Istanbul, Ekrem Imamoglu, ambaye ni mpinzani mkuu wa Rais Recep Tayyip Erdogan.
Imamoglu alikamatwa kwa mashitaka ya rushwa, hatua iliyozusha maandamano makubwa, ambapo zaidi ya watu 1,000 wamekamatwa hadi sasa. Maandamano hayo, ambayo kwa sehemu kubwa yalikuwa ya amani, yamegeuka kuwa makabiliano na polisi, ambao walitumia gesi ya machozi na maji ya kuwasha ili kudhibiti waandamanaji.
Soma pia: Mahakama ya Uturuki yaamuru kuzuiliwa kwa Meya wa Istanbul
Kukamatwa kwa Imamoglu kunachukuliwa kama hatua ya kisiasa yenye lengo la kumzuwia kuwania urais mwaka 2028. Wakati huohuo, Erdogan amewashutumu viongozi wa upinzani kwa kuvuruga utulivu wa umma na kuahidi kuwawajibisha kisiasa na kisheria kwa maandamano haya.
ufungwa kwa Imamoglu na machafuko yanayoendelea kumesababisha wasiwasi unaozidi kuhusu demokrasia ya Uturuki na hali ya uhuru wa vyombo vya habari.