Waandamanaji mkoani Sweida wataka haki ya kujitawala
16 Agosti 2025Waandamanaji wengine waliimba wakitaka uhuru wa Sweida na kuondolewa kwa Jolani, wakimaanisha Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa, ambaye jina lake akiwa kamanda wa kundi la waasi wa Kiislamu lilikuwa Abu Mohammed al-Jolani.
Wengine walibeba mabango, moja likiwa limeandikwa "haki ya kujitawala ni haki takatifu kwa Sweida", huku lingine likitaka kufunguliwa kwa njia ya msaada kutoka nchi jirani ya Jordan.
Mamlaka za Syria zaanzisha uchunguzi wa mauaji ya kimedhehebu katika jimbo la Sweida
Wakaazi wameishutumu serikali kwa kuweka kizuizi, jambo ambalo serikali hiyo imekanusha na kutaja kuingia kwa misafara kadhaa ya misaada.
Vyombo vya habari vya serikali pia vimeripoti kuingia leo kwa msafara mwingine wa msaada katika eneo hilo.
Mwezi uliopita, mamlaka ilitangaza kuundwa kwa kamati ya kuchunguza ghasia za Sweida.