Amnesty International: Waandamanaji 16 wameuawa Kenya
26 Juni 2025Matangazo
Kwa mujibu wa shirika hilo, vingi kati ya vifo hivyo vimesababishwa na polisi. Mkuu wa Amnesty International katika taifa hilo Irungu Houghton amesema, takwimu hizo zilizotolewa Jumatano usiku zimethibitishwa pia na Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya (KNCHR) ambayo awali iliripoti vifo vya watu 8.
Soma zaidi: Kumbukumbu ya mwaka mmoja wa maandamano ya Gen-Z Kenya
Duru za habari zimeripoti kuwa, polisi walitumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya waandamanaji katika mji mkuu Nairobi.
Maandamano hayo yaliyohusisha maelfu ya raia yalilenga kuadhimisha mwaka mmoja tangu yalipofanyika maandamano ya kuupinga muswada wa ongezeko la kodi ambapo takriban watu 60 waliuawa.