Vyanzo: Mpango wa kuwahamisha Wapalestina watua Afrika
14 Machi 2025Mawasiliano hayo ni sehemu ya jaribio la kutekeleza mpango wa baada ya vita uliopendekezwa na Rais Donald Trump. Haya ni kwa mujibu wa vyanzo vya Marekani.
Vikizungumza kwa sharti la kutotajwa majina, vyanzo hivyo vimesema kuwa maafisa wa Marekani na Israel wamethibitisha mawasiliano na Somalia na Somaliland huku maafisa wa Marekani pia wakithibitisha kuhusu Sudan.
Hata hivyo, vyanzo hivyo vimesema haijafahamika kuhusu hatua zilizopigwa ama kiwango cha mazungumzo hayo.
Kulingana na vyanzo hivyo, mchakato huo wa Marekani na Israel kwa nchi hizo tatu ulianza mwezi uliopita, siku chache baada ya Trump kupendekeza mpango huo kwa Gaza.
Maafisa kutoka Sudan wamesema wamelikataa ombi hilo la Marekani, huku wa Somalia na Somaliland wakiliambia shirika la habari la AP kwamba hawafahamu kuhusu mawasiliano yoyote.