CDU, SPD vya Ujerumani vyakubaliana mpango wa kifedha
5 Machi 2025Matangazo
Hayo ni wakati kukiwa na hofu kuwa Marekani inapoteza dhamira ya kushirikiana na Ulaya na jumuiya ya kujihami ya NATO. Tangazo hilo limejiri wakati wa mazungumzo makalikati ya chama cha Merz cha siasa za wastani za mrengo wa kulia la Christian Democtratic Union - CDU, pamoja na chama dada cha Bavaria cha Christian Social Union - CSU na cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto Social Democratic - SPD.
Merz alitoa tangazo hilo pamoja na Markus Sörder wa CSU na viongozi wenza wa SPD Lars Klingbeil na Saskia Esken. Amesema katika kikao cha waandishi wa habari kuwa vyama hivyo vinapanga kuwasilisha bungeni wiki ijayo mapendekezo ya kuwepo na mfuko maalum wa kiasi cha euro bilioni 500 kwa miaka 10 ijayo kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi.