Vuguvugu jipya la waasi latangazwa mashariki mwa Kongo
31 Machi 2025Kuundwa kwa vuguvugu hilo linalojulikana kama Convention for the Popular Revolution, CPR kunatokea katika wakati ambapo jeshi la Kongo linakabiliwa na kuenea kwa kiwango kisicho cha kawaida cha waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda kwingineko mashariki mwa Kongo.
Vuguvugu la CPR lina matawi ya kisiasa na kijeshi
Katika kujibu maswali kutoka kwa shirika la habari la Reuters, Lubanga alisema CPR ina matawi ya kisiasa na kijeshi, ikiwa ni pamoja na wapiganaji wenye silaha katika maeneo matatu ya Ituri.
Machafuko yazuka tena Mashariki mwa Kongo
Kulingana na Lubanga, kuleta amani katika eneo hilo kunahitaji mabadiliko ya haraka katika uongozi wa serikali na akaongeza kuwa kundi hilo bado halijaanzisha operesheni za kijeshi.
Ofisi ya rais wa Kongo haikujibu ombi la tamko kuhusu hali hiyo.