Von der Leyen yuko India kutafuta ushirikiano
28 Februari 2025Matangazo
Von der Leyen ameyasema hayo leo kabla ya kukutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi mjini New Delhi.
Kiongozi huyo wa juu katika Umoja wa Ulaya aliwasili jana India kwa ziara ya siku mbili akiwa na ujumbe wa makimishna, inayolenga kutafuta ushirikiano wa kukabiliana na Marekani ambayo ni mshirika wake wa jadi aliyeingia katika mvutano na umoja huo.
Ujumbe wa Umoja wa Ulaya unalenga kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kibiashara na India, ambayo ni nchi ya tano yenye uchumi mkubwa duniani, baada ya Rais Donald Trump kutangaza kuongeza viwango vya ushuru dhidi ya washirika na mahasimu wake.