MigogoroUlaya
Von der Leyen: Ulaya inaandaa vikwazo vipya dhidi ya Urusi
16 Mei 2025Matangazo
Bibi Von der Leyen amearifu kuhusu hatua hizo alipozungumza na waandishi habari kabla ya kuanza kwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kisiasa ya Nchi za Ulaya unaofanyika kwenye mji mkuu wa Albania, Tirana.
Amesema awamu hiyo mpya inaweza kujumuisha marufuku ya moja kwa moja ya matumizi ya bomba la kusafirisha gesi la Nord Stream, kupunguza zaidi ukomo wa bei za nishati ya Urusi na kuilenga sekta ya fedha ya nchi hiyo.
Von der Leyen amesema Rais Putin haioneshi shauku ya kutafuta amani na kwa hivyo Umoja wa Ulaya utaongeza shinikizo kupitia vikwazo vya kiuchumi.