Von der Leyen kukabiliwa na kura ya kutokuwa na imani
3 Julai 2025Matangazo
Hayo ni kufuatia hoja iliyowasilishwa siku ya Jumatano na wabunge wa siasa kali za mrengo wa kulia. Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa hatua hiyo ikashindwa kufanikiwa, hasa ikizingatiwa kuwa hoja hiyo iliungwa mkono na idadi ndogo lakini inayohitajika ya wabunge 72 wa Bunge la Ulaya , ili kupanga tarehe ya kura hiyo.
Wabunge watajadili hoja hiyo Jumatatu ijayo mjini Strasbourg Ufaransa kabla ya upigaji kura Alhamisi wiki ijayo.
Mbunge wa Romania Gheorghe Piperea aliyeanzisha hoja hiyo anamtuhumu von der Leyen kwa ukosefu wa uwazi katika mawasiliano yake na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Pfizer Albert Bourla wakati wa janga la UVIKO-19, wakati huo Umoja wa Ulaya ulipokuwa katika mjadala wa kununua chanjo za Covid.