Sheria na HakiUjerumani
Wafanyakazi katika viwanja vya ndege Ujerumani wagoma
10 Machi 2025Matangazo
Migomo zaidi katika vituo vinavyoendeshwa na serikali ya shirikisho na mamlaka za mitaa inaendelelea wiki hii huku duru ya tatu ya mazungumzo na serikali ikipangwa kufanyika siku ya Ijumaa ya wiki hii.
Soma pia:Mgomo mkubwa wa viwanja ndege waendelea Ujerumani
Mgomo huo unakadiriwa kufuta safari za ndege zaidi ya 3,400 huku watu abiria 510,000 wakiathirika na mgomo huo.
Kwa mujibu wa idara ya udhibiti wa trafiki wa ndege nchini Ujerumani, karibu safari za ndege 6,000 hufanyika kila siku katika viwanja mbalimbali vya ndege vya Ujerumani, na zaidi ya ndege 3,000 hupitia katika anga ya Ujerumani.