Vituo vya polisi Ujerumani viko katika hali mbaya mno
12 Agosti 2025"Vyoo vya zamani, kuta zenye ukungu, mifumo ya upashaji joto iliyoharibika na mapaa yanayovuja ni mambo yanayohatarisha afya za watu wetu," alisema mwanachama wa bodi ya utendaji ya GdP Hagen Husgen.
Husgen alisema uwekezaji wa ziada uliotangazwa na serikali ya Ujerumani kwa polisi wa shirikisho hautoshi.
"Tunahitaji mabilioni ya yuro kwa ajili ya uwekezaji katika vituo vyetu vya polisi," alisema Husgen.
Afisa huyo aliendelea kusema kuwa kuna mapungufu makubwa ya magari ya polisi yanayowawezesha kutoa huduma tofauti, mambo yanayolemaza kazi za polisi.
"Ni aibu kwa kweli kw apolisi kutumia magari kama haya. Magari yaliyo na viti vilivyochanika chanika na yaliyotumika kwa miaka mingi. Wananchi wanapoona hayo, polisi hawatoi picha nzuri," alisema afisa huyo.