Visa vya ubakaji vyakithiri Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
23 Juni 2025Taarifa ya shirika hilo inaonesha kiwango hicho ni mara tatu ya idadi ya visa vya unyanyasaji vilivyoripotiwa mwaka mmoja uliopita.
Kulingana na shirika hilo, kati ya mwezi Januari hadi Juni limekusanya taarifa za zaidi ya visa 478 vya unyanyasaji wa kijinsia ambavyo ni ongezeko la asilimia 249 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Mswada wa amani wawasilishwa kwa Kongo na waasi wa M23
Save the Children imesema visa 172 kati ya hivyo ni vya ubakaji dhidi ya watoto. Tangu mwezi Januari mwaka huu, raia 71,000 nchini humo wamekimbilia Burundi, ambayo ni moja ya nchi masikini zaidi duniani yenye maelfu ya wakimbizi kutokana na mizozo iliyopita.
Hali hiyo inaripotiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako mapigano yaliibuka tena mapema mwaka huu baada ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda kudhibiti sehemu kubwa ya mashariki mwa Kongo.