Ulimwengu unaadhimisha kila Aprili 2 siku ya Usonji. Ili kufahamu hasa watoto wenye usonji wanaweza kupewa malezi ya aina gani kukuza vipawa vyao, Rashid Tshilumba amezungumza na Eunice Njeru, kutoka Nakuru, Kenya, yeye ana mtoto mwenye usonji na kwanza anaeleza tofauti iliyopo kati yake na watoto wengine.