Viongozi wa Ulaya watakutana Paris kuijadili Ukraine
16 Februari 2025Hilo linafanyika wakati bara hilo likijaribu kutoa jibu la pamoja kwa Rais wa Marekani Donald Trump baada ya kuchukua msimamo katika vita vya Ukraine.
Hatua hii imechukuliwa baada ya mjumbe wa Marekani nchini Ukraine, Keith Kellogg, kusema kwamba Ulaya haitokuwa na nafasi katika meza ya mazungumzo juu ya amani ya Ukraine, baada ya Marekani kutaka majibu ya kipi Ulaya inachoweza kuchangia kuhusu hakikisho la usalama wa Kiev.
Vance asema Marekani inatafuta "amani ya kudumu" kwa Ukraine
Waziri wa kigeni wa Ufaransa Jean-Noel Barrot, amesema mkutano huo utajadili kwa kina ni msaada gani wa haraka unaohitajika Ukraine, jukumu la Ulaya katika hakikisho la usalama wa Kiev na namna ya kuimarisha usalama wa pamoja wa Ulaya.
Mataifa yaliyoalikwa ni pamoja na Uingereza, Ujerumani, Poland, Italia na Denmark.